Posts

Showing posts from December, 2020

MNEC SALIM ASAS AWAPONGEZA MUFINDI KWA KUMPIGIA KURA NYINGI RAIS JOHN POMBE MAGUFULI

Image
 MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Iringa (MNEC) Salim Asas ameipongeza Wilaya ya Mufindi, kwa kumpigia Rais John Pombe Magufuli, kura nyingi za ndio katika uchaguzi mkuu uliopita. Salim Asas ametoa pongezi hizo wakati akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya ya Mufindi. Pamoja na pongezi hizo, Salim alikemea vikali tabia ya baadhi ya watu kutumia mitandao ya kijamii kuwachafua viongozi. Katika Mkutano huo, Salim alikabidhi vyeti vya ushindi kwa kata tatu zilioongoza katika kumpigia kura Rais Magufuli. Hata hivyo, wazee wa Kimila walimvisha mavazi ya utamaduni na kumpatia jina la kihehe la Malowosa. Mbali na wazee, CCM ya Wilaya ya Mufindi ilimkabidhi Asas Tuzo ya kutambua mchango wake katika kukijenga chama cha Mapinduzi pamoja na zawadi mbalimbali. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mufindi, Daud Yasin alimkabidhi MNEC saa yenye picha yao waliyopiga siku nyingi.