IBRAHIM NGWADA; TUTASIKILIZA KERO ZA ARDHI KILA ALHAMISI YA MWISHO WA MWEZI
Meya wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada ameamua kutenga siku moja kila mwezi ka ajili ya kusikiliza kero za wananchi, kuhusu migogoro ya ardhi.
Amesema kila Alhamisi ya mwisho wa mwezi itakuwa muafaka kwake akishirikiana na wataalamu wa ardhi kuketi na kuwasikiliza wananchi wa Manispaa ya Iringa.
Ngwada alikuwa akizungumza leo katika kikao cha mabalozi wa nyumba kumi ambacho Waziri Mkuu Mstaafu na Mezi wa CCM Mkoa wa Iringa, Mizengo Pinda.
Amesema migogoro ya ardhi ni kati ya kero alizokutana tangu aapishwe kuwa Meya wa Manispaa ya Iringa.
Kero nyingine za wananchi alizoahidi kupambana nazo ni tabia ya baadhi wa watendaji wa mitaa na kata kutaka rushwa wanapotakiwa kutoa barua za dhamana.
Mh Ngwada amesema wamepania kubuni vyanzo vingi vya mapato ili kukuza uchumi wa manispaa na kuondoa tozo ndogo dogo zinazowamiza wananchi.
“Tumekubaliana kushirikiana kwa kiasi kikubwa mimi na Mbunge, Mh Jesca Msambatavangu na tumejipanga kuhakikisha kunakuwa na mabadiliko,” amesema.
Comments
Post a Comment