MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA AMALIZA ZIARA MKOA WA IRINGA KWA KUTEMBELEA IRINGA MJINI

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi na Mjumbe wa kamati kuu ya CCM taifa Komred Kheri James leo amehitimisha ziara ya kikazi Mkoani iringa katika wilaya ya iringa mjini.

Katika Ziara hiyo ya kukagua na kuimarisha Uhai wa Chama na Jumuiya pamoja na kuzungumza na mabaraza yote ya Jumuiya za CCM imekamilika kwa Mwenyekiti  kutembelea Wilaya zote za Mkoa wa Iringa ikiwemo Mufindi,Kilolo,iringa Vijijini na Iringa Mjini.

Akizungumza na wajumbe wa Halimashauri kuu ya CCM Wilaya pamoja na Wanachama Komred kheri James  ametoa pongezi kwa Viongozi na  wanachama wa CCM wa wilaya ya Iringa Mjini kwa Ushindi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 kwa kurejesha jimbo La Iringa Mjini kwa Chama Cha Mapinduzi na Ushindi wa Kata zote.

Pia komred kheri James awasihi Viongozi wa Chama na Serikali kuendeleza Umoja na Mshikamano kwa kuhudumia na kutatua  Kero mbalimbali za wananchi na kuwataka Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kuendelea kutimiza wajibu wa Kuisimamia na Kuishauri  Serikali hasa katika utekeleza wa  ahadi na Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020-2025 ili kuleta nafuu na ustawi kwa wananchi.

Aidha Komred Kheri James  amekagua kikundi cha Vijana wa Jasiliamali wa Pikipiki na Bajaji wa Mkoa wa Iringa na kuwapongeza kwa uchapakazi na kwa juhudi za kujiendeleza kukuza kikundi hicho.

Akikamilisha Ziara yake Komred kheri James amezishukuru kamati za Siasa Za Chama Cha Mapinduzi katika Wilaya zote za mkoa wa Iringa kwa kuendelea kuzilea jumuiya za Chama Cha Mapinduzi.

Katika ziara hiyo komred kheri James ameongozana na Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Brown mwangomango,katibu Wa Idara ya Uchumi na Fedha UVCCM Ndg Nelson lusekelo pamoja na wajumbe wa kamati ya utekelezaji Mkoa wa Iringa


#TukutaneKazini

Comments

Popular posts from this blog

IBRAHIM NGWADA; TUTASIKILIZA KERO ZA ARDHI KILA ALHAMISI YA MWISHO WA MWEZI

MKAKATI MKAKATINI AWAMU YA PILI KUTIKISA IRINGA

SIKU YA TATU YA ZIARA YA MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA COMRADE KHERI JAMES; ATEMBELEA IRINGA VIJIJINI

RAIS MAGUFULI KUTUA IRINGA JUMATATU, SEPTEMBA 28, 2020