SIKU YA TATU YA ZIARA YA MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA COMRADE KHERI JAMES; ATEMBELEA IRINGA VIJIJINI
Akiwa wilayani humo komred Kheri James amezungumza na Mabaraza yote ya Jumuiya za CCM wilayani humo Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Siasa Na kilimo.
Akizungumza na wajumbe wa Mabaraza hayo Komred kheri James amewasihi kuendelea kisimamia Serikali katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ili kuleta maendeleo na ustawi wa wananchi kama tulivyowaahidi katika uchaguzi Mkuu uliopita.
Aidha Komred Kheri James ametoa pongezi za dhati kwa Halimashauri ya iringa Vijijini kwa kutekeleza kwa vitendo zoezi la uwezesheji wa vijana kiuchumi jambo ambalo limechochea vijana kuwa wabunifu na kujiajiri katika shughuli mbali mbali za uzalishaji mali.
Akikamilisha ziara yake wilayani iringa Vijijini komred kheri James allipata fursa ya kutembelea Shamba la Umoja wa Vijana Igumbilo na kuona utekelezaji wa kilimo cha kisasa Cha Mahindi,Maharage na Alizeti.Akiwa shambani hapo komred kheri james amewashukuru na Kuwapongeza vijana wote kwa kuendelea kusimamia vyema shughuli za kilimo katika shamba hilo ambalo linatumika kwa uzalishaji wa Chakula kinachotumiwa na Chuo cha Umoja wa Vijana ihemi pamoja na biashara kwa ajili ya uwendeshaji wa Shughuli za Chuo ,Na amesisitiza kuwa Umoja wa Vijana utaendelea kuwa ni jumuiya ya mfano katika kufanya shughuli za uzalishaji mali kama shamba darasa kwa vijana wengine kujifunza.
Katika ziara hiyo komred kheri James ameongozana na Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Brown mwangomango,katibu Wa Idara ya Uchumi na Fedha UVCCM Ndg Nelson lusekelo pamoja na wajumbe wa kamati ya utekelezaji Mkoa wa Iringa
Kesho komred kheri James ataendelea na Ziara yake ya kuimarisha Uhai wa chama Na Jumuiya katika wilaya ya Iringa Mjini.
Comments
Post a Comment