Posts

Showing posts from March, 2021

KAMATI YA SIASA YA CCM YAENDELEA NA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAJI VIJIJINI

Image
  Kamati ya Siasa ya CCM ikiongozwa na Mwenyekiti Dr Abel Nyamahanga, inaendelea lea na ziara ya kukagua miradi ya maji Vijijini nayosimamiwa na Wakala wa Maji Safi na Mazingira Vijijini (RUWASA) Lengo okubwa la ziara hiyo ni kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya kuhakikisha wananchi vijijini wanpatiwa maji safi na salama ili kumtua mama ndoo kichwani.

MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA AMALIZA ZIARA MKOA WA IRINGA KWA KUTEMBELEA IRINGA MJINI

Image
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi na Mjumbe wa kamati kuu ya CCM taifa Komred Kheri James leo amehitimisha ziara ya kikazi Mkoani iringa katika wilaya ya iringa mjini. Katika Ziara hiyo ya kukagua na kuimarisha Uhai wa Chama na Jumuiya pamoja na kuzungumza na mabaraza yote ya Jumuiya za CCM imekamilika kwa Mwenyekiti  kutembelea Wilaya zote za Mkoa wa Iringa ikiwemo Mufindi,Kilolo,iringa Vijijini na Iringa Mjini. Akizungumza na wajumbe wa Halimashauri kuu ya CCM Wilaya pamoja na Wanachama Komred kheri James  ametoa pongezi kwa Viongozi na  wanachama wa CCM wa wilaya ya Iringa Mjini kwa Ushindi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 kwa kurejesha jimbo La Iringa Mjini kwa Chama Cha Mapinduzi na Ushindi wa Kata zote. Pia komred kheri James awasihi Viongozi wa Chama na Serikali kuendeleza Umoja na Mshikamano kwa kuhudumia na kutatua  Kero mbalimbali za wananchi na kuwataka Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kuendelea kutimiza wajibu wa Kuisimamia na K...

SIKU YA TATU YA ZIARA YA MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA COMRADE KHERI JAMES; ATEMBELEA IRINGA VIJIJINI

Image
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi na Mjumbe wa kamati kuu ya CCM taifa Komred Kheri James leo ameendelea na Ziara yake ya kikazi ya kuimarisha Uhai wa Chama na Jumuiya katika wilaya ya Iringa Vijijini Mkoa Iringa. Akiwa wilayani humo komred Kheri James amezungumza na Mabaraza yote ya Jumuiya za CCM wilayani humo Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Siasa Na kilimo. Akizungumza na wajumbe wa Mabaraza hayo Komred kheri James amewasihi kuendelea kisimamia Serikali katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ili kuleta maendeleo na ustawi wa wananchi kama tulivyowaahidi katika uchaguzi Mkuu uliopita. Aidha Komred Kheri James ametoa pongezi za dhati kwa Halimashauri ya iringa Vijijini kwa kutekeleza kwa vitendo zoezi la uwezesheji wa vijana kiuchumi jambo ambalo limechochea vijana kuwa wabunifu na kujiajiri katika shughuli mbali mbali za uzalishaji mali. Akikamilisha ziara yake wilayani iringa Vijijini komred kheri James allipata fursa ya kutembelea Shamba la Umoja wa Vijana...

SIKU YA PILI YA ZIARA; MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA, KHERI JAMES ATEMBELEA KILOLO

Image
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi komred kheri D James leo ameendelea na Ziara ya kikazi ya kuimarisha Uhai wa Chama na Jumuia mkoa wa Iringa katika Wilaya ya kilolo. Akiwa wilayani Kilolo, Komred Kheri James amehimiza umuhimu wa jamii kuendelea kuwalea,kuwainua,kuwajengea uwezo na kuwapa fursa vijana ktk shughuli na majukumu mbalimbali ya kijamii,kiuchumi na kisiasa Ili kuwaandaa kuwa raia bora na viongozi imara na wenye tija kwa Taifa.            "Jukumu la kuwalea,kuwajengea uwezo,na kuwaandaa vijana kwa maslahi ya leo na kesho ya Nchi yetu sio jambo la hiyari,ni wajibu wa lazima kwa jamii yote kwa faida ya leo na kesho ya Taifa letu" Alisema  Komred Kheri James Pia Komred kheri James  amepongeza kamati ya siasa ya Wilaya ya Kilolo ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo kwa kuanza ujenzi wa Ofisi ya CCM ya kisasa katika wilaya hiyo. Aidha komred kheri James amewatak...

KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI; BI ANGELA MILEMBE - KATIBU WA UWT MKOA WA IRINGA

Image
                               *KUELEKEA KILELE CHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI*                                                                     BI ANJELA MILEMBE                                                         KATIBU WA UWT MKOA WA IRINGA             "Tufanye kazi kwa bidii, tuendelee kuwa waadilifu na tuhakikishe tunarithisha vizazi vyetu tabia njema ili kuandaa kizazi kijacho. Mwanamke akiaminiwa na kupewa nafasi anaweza kufanya maajabu" HERI YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MACHI 8,2021

HERI JAMES; MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA AANZA ZIARA MKOANI IRINGA

Image
  Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Comrade Hery James ameanza ziara ya kikazi Mkoani Iringa ikiwa na lengo la kuimarisha Jumuiya ya Umoja wa Vijana. Katika ziara yake, Comrade Heri ametembelea wilaya ya Mufindi na kukutana na mabaraza ya Jumuiya za UWT, WAZAZI NA VIJANA. Katika ziara hiyo, kiongozi huyo wa Jumuiya ya Vijana alisisitiza upendo, umoja na mshikamano kama njia pekee ya kuendelea kukijenga chama cha mapinduzi. Amesema uchaguzi wa mwaka jana CCM ilifanikiwa kwa sababu ya ukwelina kuwataka vijana wasomi, watumie elimu yao kwa manufaa ya jamii na chama.