SIKU YA PILI YA ZIARA; MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA, KHERI JAMES ATEMBELEA KILOLO
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi komred kheri D James leo ameendelea na Ziara ya kikazi ya kuimarisha Uhai wa Chama na Jumuia mkoa wa Iringa katika Wilaya ya kilolo.
Akiwa wilayani Kilolo, Komred Kheri James amehimiza umuhimu wa jamii kuendelea kuwalea,kuwainua,kuwajengea uwezo na kuwapa fursa vijana ktk shughuli na majukumu mbalimbali ya kijamii,kiuchumi na kisiasa Ili kuwaandaa kuwa raia bora na viongozi imara na wenye tija kwa Taifa.
"Jukumu la kuwalea,kuwajengea uwezo,na kuwaandaa vijana kwa maslahi ya leo na kesho ya Nchi yetu sio jambo la hiyari,ni wajibu wa lazima kwa jamii yote kwa faida ya leo na kesho ya Taifa letu" Alisema Komred Kheri James
Pia Komred kheri James amepongeza kamati ya siasa ya Wilaya ya Kilolo ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo kwa kuanza ujenzi wa Ofisi ya CCM ya kisasa katika wilaya hiyo.
Aidha komred kheri James amewataka viongozi hao kuendelea kuwafikia wanachama, kwani kufanya hivyo kutaendelea kukisaidia Chama na jumuiya kuvuna wanachama wengi na kuendelea kuimarika.
Katika ziara hiyo komred kheri James ameongozana na Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Brown mwangomango, pamoja na wajumbe wa kamati ya utekelezaji Mkoa wa Iringa
Kesho komred kheri James ataendelea na Ziara yake ya kuimarisha Uhai wa chama Na Jumuiya katika wilaya ya Iringa Vijijini.
Comments
Post a Comment