HERI JAMES; MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA AANZA ZIARA MKOANI IRINGA
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Comrade Hery James ameanza ziara
ya kikazi Mkoani Iringa ikiwa na lengo la kuimarisha Jumuiya ya Umoja wa
Vijana.
Katika ziara yake, Comrade Heri ametembelea wilaya ya
Mufindi na kukutana na mabaraza ya Jumuiya za UWT, WAZAZI NA VIJANA.
Katika ziara hiyo, kiongozi huyo wa Jumuiya ya Vijana alisisitiza upendo, umoja na mshikamano kama njia pekee ya kuendelea kukijenga chama cha mapinduzi.
Amesema uchaguzi wa mwaka jana CCM ilifanikiwa kwa sababu ya
ukwelina kuwataka vijana wasomi, watumie elimu yao kwa manufaa ya jamii na
chama.
Comments
Post a Comment