Katibu wa Itikadi na Uenezi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mh Humphrey Polepole amesema chama hicho kimekuwa kikiendesha kampeni za kistaarabu zilizojikita katika kutoa hoja, sababu, kueleza sera pamoja na yote ambayo yanaonyesha CCM imetoka wapi na inaelekea wapi. Pia Mh Polepole amempongeza mgombea wa CCM, Rais John Pombe Magufuli kuwa mstari wa mbele katika kuendesha kampeni hizo za kistaarabu. Kiongozi huyo wa CCM amezungumza hayo leo Septemba 25, 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma. "Tunampongeza Rais Magufuli katika hilo" anasema Polepole na kluongeza; "Bahati mbaya sana wapinzani wamekuwa mstari wa mbele kutumia uongo kama nyenzo ya kampeni! uongo mkubwa, upotoshaji wa makusudi, mi nimesjindwa kuelewa lakini uzuri watanzania wanajua uongo,"