Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi na Mjumbe wa kamati kuu ya CCM taifa Komred Kheri James leo amehitimisha ziara ya kikazi Mkoani iringa katika wilaya ya iringa mjini. Katika Ziara hiyo ya kukagua na kuimarisha Uhai wa Chama na Jumuiya pamoja na kuzungumza na mabaraza yote ya Jumuiya za CCM imekamilika kwa Mwenyekiti kutembelea Wilaya zote za Mkoa wa Iringa ikiwemo Mufindi,Kilolo,iringa Vijijini na Iringa Mjini. Akizungumza na wajumbe wa Halimashauri kuu ya CCM Wilaya pamoja na Wanachama Komred kheri James ametoa pongezi kwa Viongozi na wanachama wa CCM wa wilaya ya Iringa Mjini kwa Ushindi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 kwa kurejesha jimbo La Iringa Mjini kwa Chama Cha Mapinduzi na Ushindi wa Kata zote. Pia komred kheri James awasihi Viongozi wa Chama na Serikali kuendeleza Umoja na Mshikamano kwa kuhudumia na kutatua Kero mbalimbali za wananchi na kuwataka Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kuendelea kutimiza wajibu wa Kuisimamia na K...
Meya wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada ameamua kutenga siku moja kila mwezi ka ajili ya kusikiliza kero za wananchi, kuhusu migogoro ya ardhi. Amesema kila Alhamisi ya mwisho wa mwezi itakuwa muafaka kwake akishirikiana na wataalamu wa ardhi kuketi na kuwasikiliza wananchi wa Manispaa ya Iringa. Ngwada alikuwa akizungumza leo katika kikao cha mabalozi wa nyumba kumi ambacho Waziri Mkuu Mstaafu na Mezi wa CCM Mkoa wa Iringa, Mizengo Pinda. Amesema migogoro ya ardhi ni kati ya kero alizokutana tangu aapishwe kuwa Meya wa Manispaa ya Iringa. Kero nyingine za wananchi alizoahidi kupambana nazo ni tabia ya baadhi wa watendaji wa mitaa na kata kutaka rushwa wanapotakiwa kutoa barua za dhamana. Mh Ngwada amesema wamepania kubuni vyanzo vingi vya mapato ili kukuza uchumi wa manispaa na kuondoa tozo ndogo dogo zinazowamiza wananchi. “Tumekubaliana kushirikiana kwa kiasi kikubwa mimi na Mbunge, Mh Jesca Msambatavangu na tumejipanga kuhakikisha kunakuwa na mabadiliko,” amesema.
Kamati ya Siasa ya CCM ikiongozwa na Mwenyekiti Dr Abel Nyamahanga, inaendelea lea na ziara ya kukagua miradi ya maji Vijijini nayosimamiwa na Wakala wa Maji Safi na Mazingira Vijijini (RUWASA) Lengo okubwa la ziara hiyo ni kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya kuhakikisha wananchi vijijini wanpatiwa maji safi na salama ili kumtua mama ndoo kichwani.
Mwenyekiti wa CCM Manispaa ya Iringa, Said Rubeya amesema wanaandaa hatua ya pili ya mkakati mkakatini inayolengwa kuwaeleza wananchi nini kimefanyika ndani ya siku 100 za CCM kuongoza halmashauri ya Iringa Mjini kwa kuwa na Meya. Amesema kupitia mkakati huo kamati ya siasa ya Iringa Mjini, watafanya ziara kwenye kata zote wakiongozana na Meya wa Manispaa Iringa, Mbunge Jesca Msambatavangu, Mkuu wa Wilaya ya Iringa DC Richard Kasesela. “Ni lazima tuwaambie wananchi nini kimefanyika tangu tuchukue halmashauri,” amesema.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi na Mjumbe wa kamati kuu ya CCM taifa Komred Kheri James leo ameendelea na Ziara yake ya kikazi ya kuimarisha Uhai wa Chama na Jumuiya katika wilaya ya Iringa Vijijini Mkoa Iringa. Akiwa wilayani humo komred Kheri James amezungumza na Mabaraza yote ya Jumuiya za CCM wilayani humo Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Siasa Na kilimo. Akizungumza na wajumbe wa Mabaraza hayo Komred kheri James amewasihi kuendelea kisimamia Serikali katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ili kuleta maendeleo na ustawi wa wananchi kama tulivyowaahidi katika uchaguzi Mkuu uliopita. Aidha Komred Kheri James ametoa pongezi za dhati kwa Halimashauri ya iringa Vijijini kwa kutekeleza kwa vitendo zoezi la uwezesheji wa vijana kiuchumi jambo ambalo limechochea vijana kuwa wabunifu na kujiajiri katika shughuli mbali mbali za uzalishaji mali. Akikamilisha ziara yake wilayani iringa Vijijini komred kheri James allipata fursa ya kutembelea Shamba la Umoja wa Vijana...
Mgombea wa CCM, Rais Dkt John Pombe Magufuli anatarajia kuhutumia maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Iringa, siku ya Jumatatu, Septemba 2020. Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Brown Mwangomale amesema atahutumia mamia ya wakazi wa Mkoa wa Iringa katika uwanja wa Samora, mjini Iringa. Amewakaribisha wanananchi na wanaccm wote kujitokeza kwa wingi ili kumlaki Rais Magufuli.
Comments
Post a Comment