CHUMI AFUNGA KAMPENI KWA KUAINISHA VIPAUMBELE, HANA MPINZANI MAFINGA MJINI
Chumi afunga
kampeni Mafinga Mjini kwa kuweka bayana vipaumbele vyake
1. Miundombinu ya barabara
Ni
kuhakikisha kuwa tunajenga kilomita kadhaa za lami na Taa za Barabarani ndani
ya Mji wa Mafinga.
2.
Afya,
Kukamilisha
Miradi ya ujenzi wa Kituo Cha Afya Bumilayinga, kuanza ujenzi wa Kituo Cha Afya
Kata ya Upendo na kukamilisha taratibu
za kupata vibali na vifaa Tiba ili majengo yaliyokuwa yakitumiwa na Mkandarasi
wa barabara ya Mafinga Igawa ambayo tulimuomba Mhe Rais Magufuli alipofanya
ziara hapa Mafinga yaanze kutumika kama Kituo cha Afya cha Changarawe.
2. Elimu,
a) Elimu ya
Msingi, kuhakikisha kuwa tunajenga shule ya Msingi maeneo ya Ndolezi-(Kata ya
Boma), Lumwago (Kata ya Upendo) na Iditima (Kata ya Bumilayinga)
b) Elimu ya
Sekondari -Kuhakikisha tunakamilisha ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya
Sao Hill na kuongeza majengo ya Maabara Shule ya Sekondari ya Upendo
-
kuhakikisha tunajenga Hostels/mabweni Ili kuwapunguzia watoto taabu ya kutembea
umbali mrefu kutoka na kwenda shuleni.
4. Umeme
Pamoja na kuwa tumefikisha Umeme kila kijiji na baadhi ya mitaa, bado haujafika
kila Kitongoji, hivyo jukumu la sasa ni kuhakikisha kuwa maeneo na vitongoji
vyote ambavyo havijafikiwa umeme unafika ili kuchochea shughuli za uzalishaji
Mali na Kujiongezea kipato.
5.
Maji, tunatarajia kutokana na fedha za
mkopo wa riba nafuu kutoka India dola 500m Sawa na zaidi ya trilioni 1.2,
maarufu kama Mradi wa Miji 28, sisi ni sehemu ya wanufaika wa fedha Hizi,
tunamaliza kero ya maji katika maeneo yote ya Mji wa Mafinga.
6. Uchumi,
ujasiriamali na biashara
Pamoja na
kuongeza ufanisi katika mikopo ya Vijana, Wanawake na watu wenye ulemavu,
tutahakikisha kuwa maeneo yaliyochangamka kibiashara yanaruhusiwa kufanya
biashara masaa ishirini na manne, sambamba na Kuboresha mafunzo ya ujasiriamali
na Kuboresha mazingira ya kufanyia biashara zote muhimu ikiwemo biashara ya
mazao ya misitu.
Ndio maana
tunasema kazi ni Moja tu tarehe 28 Oktoba Ku-connect Diwani wa CCM, Mbunge
Chumi afu Tunamalizia JPM-Magufuli
Comments
Post a Comment