JESCA AFUNGA KAMPENI KWA KISHINDO IRINGA MJINI, UWANJA WANONA
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini (CCM) Jesca Msambatavangu jana amefunga kampeni zake kwa kishindo baada ya umati mkubwa wa watu kufika katika uwanja wa Mwembetogwa ili kusikiliza sera zake.
Mnec na Mbunge wa Jimbo la Mtera, David Lusinde alimnadi Jesca Msambatavangu akiwataka wana Iringa kumchagua ili awawakilishe Bungeni.
Mnec wa Mkoa wa Iringa, Salim Asas aliwataka wakazi wa Mkoa wa Iringa wasifanye kosa na badala yake wahakikishe wanakipigia Chama cha Mapinduzi kwa nafasi zote.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Said Rubeya aliwashukuru wananchi wa Iringa kwa ushirikiano wao wakati wa kampeni na kuwaomba wasisahau CCM hapo kesho, siku ya uchaguzi.
Comments
Post a Comment