Kwa Kihenzile kumenoga, afungia kampeni kata ya Makungu
Mgombea wa
Jimbo la Mufindi Kusini, David Kihenzile jana alimaliza kampeni zake akiwaomba
wananchi wa jimbo hilo wampigie kura za wingi yeye, madiwani na Rais John Pombe
Magufuli.
Kihenzile
alitumia nafasi hiyo kuainisha vipaumbele vyake ikiwamo kilimo, elimu, mawasiliano,
afya na uwezeshaji.
Mnec wa Mkoa
wa Iringa, Theresia Mtewele aliongoza ufungaji huo wa kampeni akidani Ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025.
Miongoni mwa
mambo aliyozungumzia ni Afya, miundombinu, maji, elimu na michezo.
Comments
Post a Comment