MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA AMALIZA ZIARA MKOA WA IRINGA KWA KUTEMBELEA IRINGA MJINI
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi na Mjumbe wa kamati kuu ya CCM taifa Komred Kheri James leo amehitimisha ziara ya kikazi Mkoani iringa katika wilaya ya iringa mjini. Katika Ziara hiyo ya kukagua na kuimarisha Uhai wa Chama na Jumuiya pamoja na kuzungumza na mabaraza yote ya Jumuiya za CCM imekamilika kwa Mwenyekiti kutembelea Wilaya zote za Mkoa wa Iringa ikiwemo Mufindi,Kilolo,iringa Vijijini na Iringa Mjini. Akizungumza na wajumbe wa Halimashauri kuu ya CCM Wilaya pamoja na Wanachama Komred kheri James ametoa pongezi kwa Viongozi na wanachama wa CCM wa wilaya ya Iringa Mjini kwa Ushindi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 kwa kurejesha jimbo La Iringa Mjini kwa Chama Cha Mapinduzi na Ushindi wa Kata zote. Pia komred kheri James awasihi Viongozi wa Chama na Serikali kuendeleza Umoja na Mshikamano kwa kuhudumia na kutatua Kero mbalimbali za wananchi na kuwataka Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kuendelea kutimiza wajibu wa Kuisimamia na K...
Comments
Post a Comment