DC Kasesela; Wananchi endeleeni kuijengea imani na Serikali yenu
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amesema
wananchi wanapaswa kuendelea kujenga Imani kwa Serikali yao kwa sababu
inaendelea kusikiliza na kutatua kero zao.
Amesema kati ya kero zilizomfikia mezani kwake
kutoka manispaa ya Iringa ni bili kubwa za maji na ukatili wa kijinsia.
DC Kasesela alikuwa akizungumza leo katika kikao
cha mabalozi wa nyumba kumi kilichokuwa kikiongozwa na Wairi Mkuu Mtaafu, Mh Pinda.
“Kuna kero nyingine wanawake wanapigwa na waume
zao, na wanaume nao wanapigwa na wake zao, haya yote tunashughulikia,” amesema
DC Ksesela.
Aidha amewapongeza mabalozi wa CCM kwa kuipambania
CCM na kusababisha ushindi wa kishindo manispaa ya Iringa.
Comments
Post a Comment