HILARY KIPINGI AKONGA NYOYO ZA MABALOZI WA NYUMBA KUMI MASHABIKI WA YANGA ulipuka kwa shangwe!
Katibu Mwenezi wa CCM
Mkoa wa Iringa, Hilary Kipingi amesababisha makofi na vifijo huku akiacha
mashabiki wa Simba wakitulia baada ya kutoa pongezi za ushindi wa Yanga katika
mtanange uliochezwa huko Zanzibar.
Kipingi alitoa pongezi
za ushindi wa Yanga kwenye mkutano uliowakutanisha mabalozi wa CCM na Mlezi wa
CCM mkoa wa Iringa, Mh Mizengo Pinda.
“Hongera sana wana Yanga
kwa ushindi mnono wa Jana, na Simba vumilieni tu. Yanga hoyeeee!” alisema
Kipingi.
Kuhusu CCM, Kipingi amesema
mabalozi ni kati ya makundi hayo, na kwamba kundi hilo limechangia ushindi
mkubwa wa CCM.
“Mabalozi wamefanya kazi
kubwa sana, tunawapongeza sana na tunawashukuru kwa hilo,” amesema.
Comments
Post a Comment