Ibrahim Ngwada; Msiruhusu wageni kulala na watoto majumbani kwenu
Meya wa Manispaa ya Iringa,
Ibrahim Ngwada ameitaka jamii ya wakazi wa Manispaa ya Iringa kuwalinda watoto
na kutoruhusu wageni wasilale nao wakati wanapowatembelea nyumbani kwao
Amesema matukio mengi ya ukatili kwa watoto hufanywa na watu wa karibu ambao huwa wanaaminiwa na kuachwa wawe karibu na watoto hata kwenye mazingira hatarishi.
"Tusipowalinda watoto hatutapata taifa bora lenye viongozi imara, tuwalinde tangu huko nyumbani, tusiwaach walale na watoto" amesema Mh Ngwada.
Ngwada amezungumzia jambo hilo
kutokana na mkakati wake wa kuhakikisha watoto wanalindwa, kutunzwa na
kuheshimiwa.
Mh Ngwada alizungumza hayo jana wakati
wa maandalizi ya video ya wimbo wa *MTOTO WA AFRIKA* ya Dkt Tumaini Msowoya
unaosimamiwa kwa pamoja kati ya unaofanywa chini ya kampuni ya Home Studio
Production ya Arusha na SCALLET Video Production ya Jijini Dar es Salaam.
Comments
Post a Comment