JESCA MSAMBATAVANGU; *TUMEIBUKA TUKIWA NA NGUVU*
Mbunge wa Jimbo la
Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu amesema licha ya miaka kumi jimbo hilo kuwa
upinzani, CCM imeibuka tena ikiwa na nguvu.
Jesca alikuwa
akiwashukuru mabalozi wa nyumba kumi katika kikao kilichokuwa kinaongozwa na
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Amewashukuru mabalozi wa
nyumba kumi kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kuhakikisha kuwa wanasimamia ushindi
wa kishondo kwa Rais Magufuli, wabunge na madiwani.
“Mkuu wa wilaya na mkuu
wa mkoa walikuwa wanapata shuda kukusanya kero za wananchi lakini sasa tupo,
tutafanya kazi hiyo kuwapunguzia mzigo,” amesema Msambatavangu.
Comments
Post a Comment