KATIBU WA UVCCM TAIFA MWALIMU MWANGWALA AKUTANA NA VIJANA WA UVCCM IRINGA MJINI
kATIBU Mkuu wa UVCCM Taifa, Mwalimu RAYMOND MWANGWALA amekutana na kufanya mazungumzo na vijana wa UVCCM Iringa mjini.
Mwangwala amewashukuru vijana hao kwa jitihada zao za kusaidia ushindi wa Jimbo la Iringa Mjini.
Katika kikao hicho, Mwenyekiti wake Ndg Salvatory Ngerera pia aliwashukuru vijana kwa kazi kubwa walioifanya katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ambapo matokeo yake ni ushindi wa kishindo wa CCM Iringa Mjini.
Katika kikao hicho pia Umoja wa Vijana umewashukuru na kuwapa hati za pongezi viongozi na makada wote ambao wakati wote wamekuwa walezi wa vijana katika wilaya hiyo wakiongozwa na MNEC wa CCM Mkoa wa IRINGA Ndg Salim F Abri
Comments
Post a Comment