Kikao cha Mabalozi wa CCM Iringa Mjini chaibua kero ya bili kubwa ya maji.
Kikao cha Mabalozi wa CCM kimeibua kero ya bili kubwa za maji, jambo lililosababisha viongozi, akiwemo Waziri Mkuu na Mlezi wa CCM Mkoa wa Iringa, Mizengo Pinda kuzungumzia.
Hoja hiyo iliibuliwa na wananchi, hivyo Mkuu wa Wilaya ya Iringa
Mjini, Richard Kasesela, Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu kuahidi
kukutana na Waziri wa Maji, ili kutatua kero hiyo.
Awali, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dr Abel Nyamahanga,
Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Brown Mwangomale na Mwenyekiti wa CCM wa Iringa
Mjini, Said Rubeya walisema, maji imekuwa kero ambayo inapaswa kushughulikiwa.
“Utadhani tunaagiza maji China? Bili ya maji Iringa ni kubwa sana”
amesema Myamahanga.
Mbunge Jesca Msambatavangu alisema jambo hilo wameanza kulishughulikia na kwamba, kazi iliyobaki ni kwenda kwa waziri wa maji kuona walau, maji yanayotoka Iringa mjini yawe na ruzuku ili kupunguza mzigo kwa wananchi.
Comments
Post a Comment