MNEC wa Iringa, Salim Asas awavunja mbavu wabunge na madiwani, Asema Paka waliyemchagua 2017 amekamata Panya wote Iringa.
Huku akiwavunja mbavu wabunge na Madiwani wa CCM wa Mkoa wa
Iringa, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Iringa, Salim Abri Asas
amekumbushia maneno aliyotumia mwaka 2017 wakati akiomba nafasi hiyo ya
kuwaomba wajumbe, wasichague aina ya paka wanayetaka akamate panya.
Mnec alikuwa akizungumza na wabunge na wajumbe katika
Mkutano Maalum wa Wabunge na Madiwani uliokuwa unaongozwa na Waziri Mkuu
Mstaafu, Mizengo Pinda ambaye pia ni Mlezi wa CCM wa Mkoa wa Iringa.
Salim amesema aliwaambia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wa
Mkoa wa Iringa kwamba, ili ushindi upatikane katika jimbo la Iringa na kata
zenye upinzani, wasiangalie rangi ya paka atakayekamata panya.
“Niliema nitahakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo 2020,
niliwaambia ukiwa na panya hushauriwi kuchagua rangi ya Paka. Kuna panya
wanatusumbua jamani?” alihoji Salim Asas.
Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa akimkaribisha Salim Asas, Mnec wa Iringa kuzungumza na wabunge na madiwani.
Comments
Post a Comment