POKEENI SIMU ZA WANANCHI - DR NYAMAHANGA
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Dk Abel Nyamahanga
amewataka viongozi waliochaguliwa kwa kupigiwa kura kujenga tabia ya kupokea
simu za wananchi.
Nyamahanga alikuwa akizungumza kwenye kikao cha mabalozi wa nyumba
kumi waliokutana kwa ajili ya kupewa shukrani toka kwa Waziri Mkuu Mstaafu na
Mlezi wa CCM Iringa, Mizengo Pinda.
Amesema hakuna mkubwa zaidi ya wananchi waliowapa dhamana ya
kuwa viongozi kwenye maeneo yao.
“Pokeeni simu, hakuna mkubwa kwenye chama hiki , wakubwa ni
wananchi waliowachagua nyie. Fanyeni kazi na pokeeni simu,” amesema.
Amesema ipo tabia ya baadhi ya viongozi wa kata kujifanya
miungu watu wa kuwachaji fedha wananchi wanaoenda kuomba dhamana
Comments
Post a Comment