KATIBU WA CCM IRINGA, MWANGOMALE AFANYA ZIARA WILAYANI MUFINDI, KUIMARISHA UHAI WA CHAMA
Katibu wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Ndugu Brown Mwangomale amefanya ziara ya kuimarisha uhai wa chama hicho wilayani Mufindi kwa lengo la kukagua ujenzi nyumba ya katibu wa CCM wilaya ya Mufindi.
Katika ziara hiyo, Mwangomale
ambaye aliongozana na Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Iringa, Sadick Kadulo
ameagiza ujenzi wa nyumba hiyo uanze mara
moja baada ya kusimama kwa miaka mingi, bila kuendelezwa.
Pia, Mwangomale ametembelea
viwanja viwili vya CCM vilivyopo karibu na kituo cha Polisi na kuishauri CCM
Wilaya ya Mufindi kujenga hoteli ya kisasa, itakayosaidia kuongeza mapato.
Kuhusu uwanja wa Mpira, Mwangomale
ameiomba CCM Makao Makuu kusaidia ujenzi wa kisasa kwenye uwanja huo ili
kuendeleza sekta ya michezo ndani ya mkoa wa Iringa.
Comments
Post a Comment