UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM- MKOA WA IRINGA WAENDELEZA MIKAKATI KUTOKOMEZA NA UTAPIAMLO HASA KWA WATOTO
Afisa Lishe wa Mkoa wa Iringa, Neema Mtekwa amesema wanaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali katika kukabiliana na utapiamlo kwa watoto mkoani Iringa.
Mikakati hiyo inatekelezwa wakati ambapo asilimia 47 ya watoto mkoani humo wanaudumavu, asilimia 3.7 wana ukondefu na asilimia sita wana ukondefu.
Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 inasisitisha lishe bora kwa watoto na kupambana na tatizo la utapiamlo.
Miongoni mwa mikakati hiyo ni elimu kwa jamii juu ya ulaji mlo kamili, matibabu sahihi kwa wale waliopata ugonjwa huo, utoaji wa virutubisho nyongeza na unyaji wa maziwa shuleni.
Mikakati mingine ni kuhamaisha wazee wa kimila, viongozi wa dini kuzungumzia suala la lishe, kulifanya suala la lishe kama agenda kwenye vikao sambamba na kuwa na clubs za wanafunzi ili wajadili jambo hilo.
Comments
Post a Comment