UTEKELEZAJI WA ILANI; IDARA YA ELIMU MKOA WA IRINGA YAWAFIKIA WATOTO WENYE ULEMAVU
Afisa Elimu wa Mkoa wa Iringa, Germana Mung'aho amesema wanaendelea kutekeleza Ilani ya CCM kwa kuhakikisha kila mtoto anapata haki ya msingi ya kupata elimu, kwa kuwafikia watoto wenye ulemavu.
Amesema tayari wameendesha zoezi la ubainishaji wa watoto hao, na wanaandaliwa fursa ya kupata elimu kulingana na aina ya ulemavu wao.
"Kuna watoto watapelekwa kwenye elimu jumuishi na wengine elimu maalum kulingana na ulemavu wao. Sera ya watu wenye ulemavu na Ilani ya CCM vyote vinataja haki sawa kwa watoto bila ubaguzi," amesema.
Ofisa Elimu ya watu Maalum, Iringa Vijijini Vumilia Chaki, amesema hiyo ni fursa kwa watoto wenye ulemavu kupata haki zao.
"Kuna watoto ambao hawapati haki zao kwa sababu tu wapo mbali na maeneo ya shule au, kwa kuwa familia zao zina kipato duni,"amesema.
Comments
Post a Comment