Posts

Showing posts from January, 2021

MIAKA 44 YA KUZALIWA KWA CCM - UWT MKOA WA IRINGA YAANDAA MAKUBWA

Image
Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Mkoa wa Iringa umeandaa shughuli kabambe katika kuadhimisha miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM ikiwamo kupima magonjwa mbalimbali bure na uchangiaji wa damu. Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Iringa, Nikolina Luandala na Katibu wa UWT Mkoa wa Iringa, Angela Milembe wamesema maadhimisho hayo yatafanyika katika uwanja wa Mwembetogwa, February 1, 2021 kuanzia saa mbili kamili asubuhi . Magonjwa mengine yatakayopimwa ni magonjwa ya moyo,  Kisukari, saratani ya matiti na saratari ya uzazi. Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (MNEC) Salim Asas

KATIBU WA UVCCM TAIFA MWALIMU MWANGWALA AKUTANA NA VIJANA WA UVCCM IRINGA MJINI

Image
  kATIBU Mkuu wa UVCCM Taifa, Mwalimu RAYMOND MWANGWALA amekutana na kufanya mazungumzo na vijana wa UVCCM Iringa mjini. Mwangwala amewashukuru vijana hao kwa jitihada zao za kusaidia ushindi wa Jimbo la Iringa Mjini. Katika kikao hicho, Mwenyekiti wake Ndg Salvatory Ngerera pia aliwashukuru  vijana kwa kazi kubwa walioifanya katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ambapo matokeo yake ni ushindi wa kishindo wa CCM Iringa Mjini. Katika kikao hicho pia Umoja wa Vijana umewashukuru na kuwapa hati za pongezi viongozi na makada wote ambao wakati wote wamekuwa walezi wa vijana katika wilaya hiyo wakiongozwa na MNEC wa CCM Mkoa wa IRINGA Ndg Salim F Abri

Ibrahim Ngwada; Msiruhusu wageni kulala na watoto majumbani kwenu

Image
  Meya wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada ameitaka jamii ya wakazi wa Manispaa ya Iringa kuwalinda watoto na kutoruhusu wageni wasilale nao wakati wanapowatembelea nyumbani kwao Amesema matukio mengi ya ukatili kwa watoto hufanywa na watu wa karibu ambao huwa wanaaminiwa na kuachwa wawe karibu na watoto hata kwenye mazingira hatarishi. "Tusipowalinda watoto hatutapata taifa bora lenye viongozi imara, tuwalinde tangu huko nyumbani, tusiwaach walale na watoto" amesema Mh Ngwada. Ngwada amezungumzia jambo hilo kutokana na mkakati wake wa kuhakikisha watoto wanalindwa, kutunzwa na kuheshimiwa. Mh Ngwada alizungumza hayo jana wakati wa maandalizi ya video ya wimbo wa *MTOTO WA AFRIKA* ya Dkt Tumaini Msowoya unaosimamiwa kwa pamoja kati ya unaofanywa chini ya kampuni ya Home Studio Production ya Arusha na SCALLET Video Production ya Jijini Dar es Salaam.  

Uhai wa CCM; Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa akikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya CCM Kilolo na nyumba ya UVCCM

Image
  Ukizungumzia uhai wa chama ni pamoja na uwepo wa ofisi nzuri na nyumba za watendaji. Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Brown Mwangomale na viongozi wengine wa CCM Mkoa wa Iringa, wamefanya ziara kukagua nyumba ya Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Iringa na Ofisi ya CCM Wilaya ya Kilolo.  

HILARY KIPINGI AKONGA NYOYO ZA MABALOZI WA NYUMBA KUMI MASHABIKI WA YANGA ulipuka kwa shangwe!

Image
  Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Iringa, Hilary Kipingi amesababisha makofi na vifijo huku akiacha mashabiki wa Simba wakitulia baada ya kutoa pongezi za ushindi wa Yanga katika mtanange uliochezwa huko Zanzibar.   Kipingi alitoa pongezi za ushindi wa Yanga kwenye mkutano uliowakutanisha mabalozi wa CCM na Mlezi wa CCM mkoa wa Iringa, Mh Mizengo Pinda.   “Hongera sana wana Yanga kwa ushindi mnono wa Jana, na Simba vumilieni tu. Yanga hoyeeee!” alisema Kipingi.   Kuhusu CCM, Kipingi amesema mabalozi ni kati ya makundi hayo, na kwamba kundi hilo limechangia ushindi mkubwa wa CCM.   “Mabalozi wamefanya kazi kubwa sana, tunawapongeza sana na tunawashukuru kwa hilo,” amesema.

JESCA MSAMBATAVANGU; *TUMEIBUKA TUKIWA NA NGUVU*

Image
  Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu amesema licha ya miaka kumi jimbo hilo kuwa upinzani, CCM imeibuka tena ikiwa na nguvu.   Jesca alikuwa akiwashukuru mabalozi wa nyumba kumi katika kikao kilichokuwa kinaongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.   Amewashukuru mabalozi wa nyumba kumi kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kuhakikisha kuwa wanasimamia ushindi wa kishondo kwa Rais Magufuli, wabunge na madiwani.   “Mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa walikuwa wanapata shuda kukusanya kero za wananchi lakini sasa tupo, tutafanya kazi hiyo kuwapunguzia mzigo,” amesema Msambatavangu.        

DC Kasesela; Wananchi endeleeni kuijengea imani na Serikali yenu

Image
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amesema wananchi wanapaswa kuendelea kujenga Imani kwa Serikali yao kwa sababu inaendelea kusikiliza na kutatua kero zao. Amesema kati ya kero zilizomfikia mezani kwake kutoka manispaa ya Iringa ni bili kubwa za maji na ukatili wa kijinsia. DC Kasesela alikuwa akizungumza leo katika kikao cha mabalozi wa nyumba kumi kilichokuwa kikiongozwa na Wairi Mkuu Mtaafu, Mh Pinda. “Kuna kero nyingine wanawake wanapigwa na waume zao, na wanaume nao wanapigwa na wake zao, haya yote tunashughulikia,” amesema DC Ksesela. Aidha amewapongeza mabalozi wa CCM kwa kuipambania CCM na kusababisha ushindi wa kishindo manispaa ya Iringa.

IBRAHIM NGWADA; TUTASIKILIZA KERO ZA ARDHI KILA ALHAMISI YA MWISHO WA MWEZI

Image
  Meya wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada ameamua kutenga siku moja kila mwezi ka ajili ya kusikiliza kero za wananchi, kuhusu migogoro ya ardhi. Amesema kila Alhamisi ya mwisho wa mwezi itakuwa muafaka kwake akishirikiana na wataalamu wa ardhi kuketi na kuwasikiliza wananchi wa Manispaa ya Iringa. Ngwada alikuwa akizungumza leo katika kikao cha mabalozi wa nyumba kumi ambacho Waziri Mkuu Mstaafu na Mezi wa CCM Mkoa wa Iringa, Mizengo Pinda. Amesema migogoro ya ardhi ni kati ya kero alizokutana tangu aapishwe kuwa Meya wa Manispaa ya Iringa. Kero nyingine za wananchi alizoahidi kupambana nazo ni tabia ya baadhi wa watendaji wa mitaa na kata kutaka rushwa wanapotakiwa kutoa barua za dhamana. Mh Ngwada amesema wamepania kubuni vyanzo vingi vya mapato ili kukuza uchumi wa manispaa na kuondoa tozo ndogo dogo zinazowamiza wananchi. “Tumekubaliana kushirikiana kwa kiasi kikubwa mimi na Mbunge, Mh Jesca Msambatavangu na tumejipanga kuhakikisha kunakuwa na mabadiliko,” amesema.

POKEENI SIMU ZA WANANCHI - DR NYAMAHANGA

Image
  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Dk Abel Nyamahanga amewataka viongozi waliochaguliwa kwa kupigiwa kura kujenga tabia ya kupokea simu za wananchi. Nyamahanga alikuwa akizungumza kwenye kikao cha mabalozi wa nyumba kumi waliokutana kwa ajili ya kupewa shukrani toka kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mlezi wa CCM Iringa, Mizengo Pinda. Amesema hakuna mkubwa zaidi ya wananchi waliowapa dhamana ya kuwa viongozi kwenye maeneo yao. “Pokeeni simu, hakuna mkubwa kwenye chama hiki , wakubwa ni wananchi waliowachagua nyie. Fanyeni kazi na pokeeni simu,” amesema. Amesema ipo tabia ya baadhi ya viongozi wa kata kujifanya miungu watu wa kuwachaji fedha wananchi wanaoenda kuomba dhamana

MKAKATI MKAKATINI AWAMU YA PILI KUTIKISA IRINGA

Image
  Mwenyekiti wa CCM Manispaa ya Iringa, Said Rubeya amesema wanaandaa hatua ya pili ya mkakati mkakatini inayolengwa kuwaeleza wananchi nini kimefanyika ndani ya siku 100 za CCM kuongoza halmashauri ya Iringa Mjini kwa kuwa na Meya. Amesema kupitia mkakati huo kamati ya siasa ya Iringa Mjini, watafanya ziara kwenye kata zote wakiongozana na Meya wa Manispaa Iringa, Mbunge Jesca Msambatavangu, Mkuu wa Wilaya ya Iringa DC Richard Kasesela. “Ni lazima tuwaambie wananchi nini kimefanyika tangu tuchukue halmashauri,” amesema.  

Magufuli ni kiongozi wa aina yake ; Mh Mizengo Pinda

Image
  Mlezi wa CCM Mkoa wa Iringa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizngo Pinda amesema watanzania wana kila sababu ya kuendelea kumuombea Rais John Pombe Magufuli kwa sababu ni kiongozi wa aina yake. Mh Pinda alikuwa akizungumza kwenye kikao kilicho wakutanisha mabalozi wa Jimbo la Iringa Mjini kikiwa na lengo la kuwashukuru. Amesema kazi alizofanya Rais Magufuli ndizo zilizosababisha uchaguzi wa mwaka jana ufanikiwe kwa kiwango kikubwa. “Amefanya kazi kubwa sana na hicho kimechochea ushindi wa CCM, tumuombee sana,” amesema .

Kikao cha Mabalozi wa CCM Iringa Mjini chaibua kero ya bili kubwa ya maji.

Image
Kikao cha Mabalozi wa CCM kimeibua kero ya bili kubwa za maji, jambo lililosababisha viongozi, akiwemo Waziri Mkuu na Mlezi wa CCM Mkoa wa Iringa, Mizengo Pinda kuzungumzia. Hoja hiyo iliibuliwa na wananchi, hivyo Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela, Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu kuahidi kukutana na Waziri wa Maji, ili kutatua kero hiyo. Awali, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dr Abel Nyamahanga, Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Brown Mwangomale na Mwenyekiti wa CCM wa Iringa Mjini, Said Rubeya walisema, maji imekuwa kero ambayo inapaswa kushughulikiwa. “Utadhani tunaagiza maji China? Bili ya maji Iringa ni kubwa sana” amesema Myamahanga. Mbunge Jesca Msambatavangu alisema jambo hilo wameanza kulishughulikia na kwamba, kazi iliyobaki ni kwenda kwa waziri wa maji kuona walau, maji yanayotoka Iringa mjini yawe na ruzuku ili kupunguza mzigo kwa wananchi. Hoja ya kumuona waziri, ilizungumzwa pia na Mh Kasesela  aliyesema kero hiyo imemfikia ...

RC Hapi awasihi wabunge, Madiwani kutekeleza wajibu wao

Image
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi amesema amewaomba wabunge na madiwani kutekeleza  majukumu yao badala ya kuiachia Serikali peke yake. Amesema awali walikuwa wakilazimika kufanya kazi kama wabunge na madiwani lakini ushindi wa CCM utasaidia kila aliyechaguliwa kutekeleza wajibu wake. Mh Hapi alikuwa akizungumza kwenye kikao maalum cha wabunge na madiwani kilichofanyika leo, kikiongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mh Mizengo Pinda ambaye ni mlezi wa CCM wa Mkoa wa Iringa.

Dk Nyamahanga ; 2025 tusijiandae kwa maneno

Image
Mwenyekiti wa CCM w Mkoa w Iringa, Dk Abel Nyamahanga amewashauri wabunge na madiwani wa CCM wa Mkoa wa Iringa kushikamana na kushirikiana katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010. Amesema mwisho wa Uchaguzi ni mwanzo wa Uchaguzi mwingine hivyo 2025 siyo ya kujiandaa kwa maneno bali kwa vitendo. “Hata kama huna mpango wa kugombea 2025, chapa kazi kuihakikishia ushindi CCM” alisema. Dk Nyamahanga alikuwa akizungumza wenye kikao maalum cha Wabunge na Madiwani wa CCM wa Mkoa wa Iringa kilichokuwa kinaongozwa na Mlezi wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Mh Mizengo Pinda.  

WAZIRI MKUU STAAFU, MIZENGO PINDA AWAFUNDA WABUNGE NA MADIWANI WA IRINGA

Image
  Mlezi wa CCM Mkoa wa Iringa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda amewafunda wabunge wa Majimbo ya Mkoa wa Iringa na madiwani wote wa CCM k kutobweteka, badala yake wafanye kazi kwa bidii ili chama hicho kishinde tena 2025. Mh Pinda alikuwa akizungumza leo katika kikao Maalum cha Madiwani na Wabunge wa CCM wa Mkoa wa Iringa kilichokuwa na lengo la kutoa maelekezo ya namna ya kutekelea Ilani ya Uchaguzi ya 2020. Amesema kazi ya sasa ni kuhakikisha Ilani ya CCM inatekelezwa kwa kiwango cha juu ili mwaka 2025 chama cha Mapinduzi kisipate kazi ngumu. Hata hivyo amesema, wakati huu upinzani ulikuwa dhaifu jambo lililosababisha kuwa na mazingira mazuri ya ushindi. Alitaja mambo muhimu kwenye ilani kuwa ni kuendeleza jitihada za kudumisha Muungano, kusimamia maadili na miiko ya uongozi, kutenga muda wa kusikiliza kero za wananchi na kujenga mahusiano kwa kutojifanya wakubwa kwa waliowachagua.

MNEC wa Iringa, Salim Asas awavunja mbavu wabunge na madiwani, Asema Paka waliyemchagua 2017 amekamata Panya wote Iringa.

Image
 Huku akiwavunja mbavu wabunge na Madiwani wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Iringa, Salim Abri Asas amekumbushia maneno aliyotumia mwaka 2017 wakati akiomba nafasi hiyo ya kuwaomba wajumbe, wasichague aina ya paka wanayetaka akamate panya. Mnec alikuwa akizungumza na wabunge na wajumbe katika Mkutano Maalum wa Wabunge na Madiwani uliokuwa unaongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda ambaye pia ni Mlezi wa CCM wa Mkoa wa Iringa. Salim amesema aliwaambia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wa Mkoa wa Iringa kwamba, ili ushindi upatikane katika jimbo la Iringa na kata zenye upinzani, wasiangalie rangi ya paka atakayekamata panya. “Niliema nitahakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo 2020, niliwaambia ukiwa na panya hushauriwi kuchagua rangi ya Paka. Kuna panya wanatusumbua jamani?” alihoji Salim Asas. Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa akimkaribisha Salim Asas, Mnec wa Iringa kuzungumza na wabunge na madiwani.

MWANGOMALE; TUTATOA TUZO KATA YA KIYOWELA KWA USHINDI WA ASILIMIA 100

Image
Katibu wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Brown Mwangomale amesema watatoa Tuzo ili kuipongeza kata ya Kiyowela, katika Jimbo la Mufindi Kusini, kwa kupata ushindi wa asilimia 100 wa kura za Rais John Magufuli. Mwangomale amesema hayo katika kikao maalum cha Wabunge wote na madiwani wa CCM wa Mkoa a Iringa, kinachoongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinga ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Iringa. Mwangomale amesema, kata hiyo inaweza kuwa ya kwanza kitaifa kwa kuwa kwa kuwa na wapiga kura wote waliojiandikisha kushinda kwa kishindo. Kutokana na ushindi huo, Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi James Mgego amesema ushindi huo unatokana na ushirikiano mkubwa baina ya chama na Serikali wilayani Mufindi. “Pia ni wilaya yenye katibu kijana kuliko wote,” amesema Mgego. Mufindi kusini imeshika nafasi ya kwanza, Kilolo ya pili na Kalenga nafasi ya tatu.

MH MIZENGO PINDA AONGOZA KIKAO MAALUM CHA WABUNGE NA MADIWANI WOTE WA CCM IRINGA

Image
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh Mizengo Pinda ameongoza kikao maalum cha Wabunge na Madiwani wote wa CCM wa Mkoa wa Iringa. Katika kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mh Ally Hapi na wakuu wote wa wilaya walihudhuria. Pia, Sekretarieti za CCM za Wilaya zote za Mkoa wa Iringa pamoja na Mkoa wa Iringa zimehudhuria lengo likiwa maelekezo maalum ya utekelezaji wa Ilani ya CCM pamoja na kupongeza ushindi wa kishindo wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka jana.